Leo katika pita pita zangu kama ilivo kawaida yangu ya kupiga picha mandhari mbali mbali, kiukweli niliweza kuvutiwa na muonekano wa sehemu hizi na kwa maana hiyo basi nikaamua kushare na wewe kile ambacho nimekiona.
Hakika Dodoma ina sehemu nyingi na nzuri miongoni mwa sehemu hizo hadi sasa bado kuna kumbukumbu ya enzi za mababu zetu.
Mfano: Kondoa Irangi ambapo panajulikana kwa umaarufu wake wa Michoro ya Mapangoni. Sijawahi kutembelea ila natumai tafanya hivo siku moja.
Baadhi ya picha nilizopiga ni hizi hapa, unaweza kuona kuwa picha hazina ubora mzuri sana lakini zinakidhi viwango, kwasababu picha hizi zimepigwa kwa kutumia
Camera ya simu na sio
DSLR Camera. Ila nimezifanyia marekebisho kidogo ziweze kuwa na mwonekano mzuri zaidi.
 |
Dodoma Tanzania - Reli ya kati |
Hapo juu ni picha ya Reli ya kati, kiukweli ni moja ya picha ambayo inavutia na napenda kuiangalia. Nilipiga picha hii nikiwa nimesimama na hicho ndicho kilichotokea.
 |
Dodoma Tanzania - Reli |
Hiyo ni picha ya Reli ya kati ambayo nilipiga kwa upande mmoja, hapo nililaza Camera yangu ya simu kwa ukaribu zaidi kiasi kwamba ilikuwa inakaribia kugusa chini. Ni picha niliopiga kwa umakini na ustadi wa hali ya juu.
 |
Dodoma - Daraja la JR |
Moja ya picha zangu nzuri nazozifurahia na hii ipo pia. Picha hii nimeipiga kwa ustadi zaidi na nikiweka focus zaidi kwenye vitu vitatu, Reli, Daraja na Horizon.
 |
Dodoma Tanzania - Shamba la Bibi |
Nimependa kuita hiyo picha shamba la bibi kwasababu ni wakati napiga alikuwapo bibi mmoja anafanya kazi zake kwenye shamba hilo. Ila lengo langu halikuwa kupiga picha ya shamba bali ni Horizon.
 |
Dodoma Tanzania - Mto Udom |
Picha hii nimeichukulia kama mto kwani kilicho kwenye focus kwa hali ya kawaida kinaonekana kama mto, ila hii ni njia ambayo watu hupita ila hua haipitiki mvua zikinyesha kwani maji hukatiza.
Na hii ni Reli pia ila kwa upande kuu inaelekea Dar Es Salaam. Ni picha ambayo inapendeza kuweka kama wallpaper kwenye simu au computer.
 |
Wallpaper - Samsung |
Picha hiyo imepigwa Juu ya gorofa ila simu hiyo kwenye focus iliwekwa dirishani.
 |
UDOM - Informatics |
Na hii ni picha ya College Of Informatics And Virtual Education (CIVE). Picha hii ilipigwa nikiwa nimesimama na kuchukua jengo la utawala. Picha hii imepigwa kipindi cha masika Mwezi wa 3/2018
Hiyo hapo juu ni picha ya Dirisha. Kwa mbele unaweza kuona ni majengo ya Hostels za wanafunzi (CIVE).
Zipo Picha nyingi na nzuri ambazo huwa napiga kwa kutumia simu yangu. Pia takuwa nikishare nayi tafiti mbali mbali ambazo nazifanya. Tembelea Blog yangu mara kwa mara.
SALUTE UMETISHA KAKA
ReplyDeletePamoja sana my friend, appreciate you sana.
DeleteAsante sana mkuu
ReplyDelete