Full width home advertisement

Graphics

Tech News

Post Page Advertisement [Top]

Ikiwa unatumia Wi-Fi kuunganisha computer yako kwenye internet basi lazima kutakuwa na updates za hapa na pale kuwezesha Windows Operating system yako kwenda na wakati. Japo ni za muhimu hizo updates yamkini hauhitaji kufanya update kwa muda huo ila windows inakulazimisha kufanya hivo.

 Basi kuna njia rahisi ya kuzuia updates kwenye Operating system yako kwa kutumia Metered Connection ukiwa umeunganisha kwenye Wi-Fi network.
Metered Connection: Ni network ambayo inakuwa na limit ya data. Unapofanya network yako kama Metered connection unazuia Automatic updates ya Windows pia inakusaidia kupunguza matumizi ya data kwenye computer yako kwa baadhi ya Apps.

Jinsi ya Kutoa Auto Updates Ya Windows Kwenye Wi-Fi
Fuata njia zifuatazo.
1. Unganisha Computer kwenye Network (Mfano Wi-Fi ya simu)
Connect kwenye WiFi network
2. Fungua All Settings. bonyeza icon ya Notification. Au tumia shortcut (Windows key + i) kwenye keyboard yako. Pia unaweza kutumia Windows key kisha bofya Settings.
All Settings
3. Nenda kwenye Network and Internet, itakupeleka hadi kwenye Wi-Fi na setting nyingine. 
Network and Internet
4. Ukiwa kwenye Wi-Fi Bofya Advancesd Options, kama inavoonesha kwenye picha hapo chini.
Advanced Options
5. Angalia Metered Connection baada ya kufungua Advanced Options.
Kama iko Off bonyeza switch kuwasha na kufanya network yako metered connection, kama iko on basi unaweza iacha kama ilivo.
Kuwasha Metered connection

Baada ya hapo utakuwa umezuia Auto Update kwenye computer yako. Kwani Metered connection inakusaidia kufanya hivo.

MUHIMU: Share na comment pia kama utakuwa umepata tatizo.



Mawasiliano:
Instagram: mdaki.jr
Phone: +255 628 420 222

2 comments:

  1. Replies
    1. Skukrani sana my friend Ramay. Tuko pamoja sana. Najitahidi kuweka quality contents iwezekanavyo, uskose post mpya subscribe kwa email yako.

      Delete

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib