Full width home advertisement

Graphics

Tech News

Post Page Advertisement [Top]

Faida za kuroot simu ni nyingi, na nitakuelezea kwa undani zaidi. Ila kabla ya yote ni vema kujua kwanza maana yenyewe ya Root kabla ya kuendelea. ROOT kwa lugha ya kiswahili ni MZIZI. Hivo basi hata katika Computer root ina maana hiyo hiyo ya mzizi yaani mwanzo kabisa wa utengenezaji wa mafile ambayo yanaiongoza Computer.

Katika simu ni jina la account au mtumiaji ambaye ana uwezo wa kuamuru (Commands) na kuyapata ma file ambayo yapo kwenye simu yako. Kwa kawaida huwezi kuyaona au kuingiliana na file zozote ambazo zipo kwenye simu yako kama simu yako. Hivo basi unapo root simu yako ya Android ni kujipa uwezo wa kuiamuru simu yako na kuwa wewe kama kiongozi wa kila linalotokea hivo unakuwa na uwezo mkubwa  (Admin). 
Mfano mzuri ni kama "kumiliki gari ilhali bado hujajua kuendesha". Hivo wewe utakuwa ni mtu wa kuendeshwa tu, hiyo ni sawa na kutumia simu ambayo haijawa rooted. Ila "ukishajua kuliendesha gari lako", basi huo ni mfano wa simu ambayo iko rooted.

MdakiJunior - Root Simu


Je faida zipi nazipata nikiroot simu yangu?
Unapo root simu basi unakuwa mmiliki kamili wa simu yako. Kama nilivotangulia kusema hapo mwanzo zipo faida nyingi za kuroot simu. Baadhi ya hizo faida ni hizi.
  1. Kufungua features ambazo zinakuwa zimefichwa kutoka kiwandani. Hivo unkuwa na uwezo wa kufanya chocho kwenye simu yako. Kama vile kubadilisha themes na vitu vingine vingi.
  2. Uwezo wa kubadilisha muonekano wa simu yako. Unaporoot simu basi unakuwa na uwezo wa kubadilisha muonekano wa simu kwa kubadilisha framework na vitu ambavyo vitabadilisha tabia (behaviour) ya system yako ya simu.
  3. Uwezo wa kubadilisha Version mpya ya Android. Kama ulikuwa unatumia Android version 4.1.2 au nyingine kama hiyo basi uki root simu unaweza badili Version na kuweka ile ambayo iko kwa wakati juo.
  4. Kupata kuifikia na kuiona Kernel ambayo ndio component ya muhimu kabisa ya Operating System ya Android yako. ambayo ina simamia (manage) mawasiliano kati ya Software na Hardware.
  5. Zuia matangazo kwenye Application zote unazo download katika simu yako. Hii inanivutia hata mimi kwani zipo baaadhi ya apps zinakera kwa kuweka matangazo kibao, hivo ukiroot simu unaweza lizuia hili.
  6. Inakupa uwezo wa kumanage application zako. Kama vile uwezo wa  kuzibadilisha (Edit), Backup na kurestore. 
Na nyingine kibao zinapatikana.

Hasara za ku root simu zi zipi?
Kila lenye faida basi ujue lazima liwe na hasara. Ila uki root simu yako unatoa warrant na unaoneza nafasi za "kubrick" simu yako. Brick ni kupata madhara kidogo wakati wa kuflash kama unataka kuifalsh simu yako kwa badae. Sio tatizo kuwa kwan simu yako inapokua break inakua inasumbua kwenye kuwaka inakuwa hiwaki vizuri. Ni tatizo ambalo linaweza kurekebishwa.

Kama una maswali au tatizo comment hapo chini tutayatatua.


MUHIMU: 

4 comments:

  1. Ku root simu inawezekana kufanyika kwenye simu yenyewe au ni mpaka kwenye computer (hiyo software ya root inawez ikafanya kazi kwenye simu au ni kwenye computer pekeake...)

    ReplyDelete
  2. Kwanini rooted simu haisaport baadhi ya file mfani m pesa au NMB app?

    ReplyDelete

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib