Full width home advertisement

Graphics

Tech News

Post Page Advertisement [Top]

Hacker ni neno la kiingereza lenye maana ya mtu anaeweza kuchukua taarifa zako za muhimu mfano password na username na kuzitumia kuingia kwenye system kufanya jambo alilokusudia. Hacker wako haraka na kwa muda mfupi wanaweza kuingia kwenye website yako ay system na kuchukua taarifa za muhimu kutoka kwenye website. Hasa ikiwa website yako inahusu watumiaji ambao wanaweka taarifaf za kifedha n.k Website ni kama mwili wa binadamu kwani usipoifanyia matunzo uwezekano wa kushambuliwa na marahi ni rahisi sana vivo hivyo kwa website kushambuliwa na hackers.

Kuiba sio wazo pekee la hacker, ila kuna mambo mengi ambayo hacker huwa anayawaza kabla ya kuhack website yako. Miongoni ni kuharibu jina lako au kufuta record, kufikisha ujumbe ili watu wanaotembelea website yako waweze kuona ujumbe huo n.k
image
MdakiJunior - Kulinda website yako na hacker
Huwa ni vigumu kurudisha website yako kama ilivokuwa mwanzo kabla haijahackiwa. Ila unaweza kujilinda hili jambo lisijitokeze.

Tips za kujilinda na hackers
1. Nenda na wakati (Updated). Tambua njia ambazo zinazoweza kuiweka website yako matatani. Pia update kila kitu kwenye system yako.

2. Imarisha Access Control, hakikisha sehemu ya admin inakuwa na ulinzi wa kutosha, kwani sehemu ya admin ndio sehemu pekee ambayo kama haiko vizuri inaweza leta madhara kwenye website yako endapo hacker atakuwa na uwezo wa kupata password na username. Pia weka kikomo cha kulogin kwenye system.

3. Weka ulinzi wa kutosha kwenye Network yako.
  • Weka expire fupi baada ya kulog out
  • Tumia password imara na ngumu kuhisi.
  • Badili password mara kwa mara
  • Scan hardware zote ambazo utaziweka kwenye system.
4. Weka WAF (Web Application Firewall), hii inatumika kusoma kila data inayopita. Inakaa kati ya server na data cocnnection.

5. Ficha page za Admin zisionekane, hauhitaji page za admin kuweza kuonyeshwa na search engines endapo mtu atasearch mfano google, bing au yahoo! Hivo tumia "robots_txt" file.

6. Weka kikomo cha kuapload mafile, kwa asilimia kubwa mafile yanayowekwa na watumiaji wa website yako yanachangia kwa kiasi kikubwa katika kuhack website. Mafile kama picha, audio au video yanakuwa yamewekewa script ambazo zinaenda kuharibu au kubadili utaratibu kwenye server yako.
7. Tumia SSL (Secure Socket Layer), hii inafanya encription hivo kuzuia taarifa kutosomwa na wasiohusika nazo.
8. Ondoa Autofill kwenye form, autofill inamrahisishia hacker kazi ya kuhack kwa kumpa vichaguzi (suggestion).
9. Fanya backup ya mara kwa mara.
10. Tumia muda wako kujielimisha zaidi.

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib