Full width home advertisement

Graphics

Tech News

Post Page Advertisement [Top]

iTunes ni program iliyotengenezwa na Apple ambayo unaweza kuitumia kwa kuplay audio. Pia inakupa nafasi ya kuangalia movies, Tv shows  mbali mbali au kudownload audio kutoka store kwa bei poa. Unaweza itumia iTunes ukiwa na bidhaa ya apple kama vile Apple laptop, iPod, tablet, smartphone n.k. Kutumia iTunes kwenye Windows computer hauhitaji uwe na Apple Id, bali unweza install na kuanza kutumia kama player ya kawaida.

images
MdakiJunior - Jinsi ya kutumia iTunes kwenye Windows Pc.

Mahitaji ili kuweka iTunes kwenye pc yako.
Hakikisha Hardware yako ina vitu vifuatavyo.
  1. Processor yenye ukubwa wa 1Ghz Intel au AMD au zaidi pia inasapoti SSE2 (Streaming SIMD Extension 2), SIMD (Single Instruction Multiple Data) hii inaelezea computer zenye processor zaidi ya moja.
  2. RAM yenye ukubwa wa 512MB.
  3. Kuplay video za kawaida kwenye iTunes unahitaji Intel poentium D au zaidi inasapoti DirectX9 video card.
  4. Kuplay 720p HD videos kwenye iTunes unahitaji 2Ghz intel Core 2 Duo na RAM 1GB na intel GMX 3000, ATI Radeon HD 2400. 
  5. Kuplay 1080p HD videos kwenye iTunes unahitaji 2.4Ghz intel Core 2 Duo au zaidi, RAM ya 2GB. NVIDIA GeForce video card.
  6. Screen yako iwe na ukubwa wa 1024x768 au zaidi.
  7. Sound Card 16-bit.
  8. Uwe na internet kwa ajili ya kuunganisha.
  9. Uwe na Windows 7 au zaidi kwenye computer yako.
Ikiiwa computer yako inasaport vitu hivyo au zaidi basi unaweza tumia iTunes kwenye computer yako yenye windows operating system.

Faida za kuwa na iTunes kwenye computer yako.
  • Inakusaidia kufanya updates au restore bidhaa za Apple. Mfano, iPod.
  • Inakusaidia kuunganisha simu yako na computer yako.
  • Inakusaidia kurusha muziki kutoka kwenye computer yako kwenda kwenye simu yako ya Apple.
Kudownload iTunes kwa computer yako Bofya hapa

 

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib