Biashara ni kazi au huduma ambayo anafanya mtu ikiwa na lengo la uzalishaji, yaani kupata kipato kutokana na hiyo shughuli anayofanya. Zipo aina nyingi za biashara katika makala ijayo tazielezea kwa undani zaidi.
Je Ni Lipi wazo zuri la Biashara?
Wazo zuri la Biashara ni lile ambalo limekujia kwa muda huo kulingana na mahitaji ya watu wanaokuzunguuka kwa muda huo. Na maana kuwa kama umeona kuna uhitaji wa kuanzisha huduma fulani ambayo watu wanahitaji basi hilo ni wazo zuri la biashara.
Sina wazo nifanye nini?
Yamkini hauna wazo la biashara na unahitaji kufanya Biashara. Njia bora ya kupata wazo zuri la biashara ni kuangalia mahitaji ya watu wako. Pia unaweza chagua wazo kwa kuzingatia muongozo huu.
1. Ni vitu gani watu wanahitaji kila siku na ni vipi huwa ni vya msimu tu. Mfano: Kila siku lazima mtu anunue unga kupika ugali. Na sio lazima kila siku anunue dawa ya meno.
2. Ni nini watu wanapenda. Mfano: Watu wanapenda kupumzika baada ya kazi kupata kinywaji baridi.
3. Ni huduma zipi watu wanahitaji kila siku. Mfano: Lazima watu wasafiri kila siku.
4. Bidhaa zipi zinanunuliwa sana na ni nani wananunua. Mfano: Vocha inanunuliwa kila siku. Watoto wanahitaji soda kila siku.
5. Ni yapi mahitaji ya wanawake, ya wanaume, ya watoto au ya wote kwa ujumla. Mfano: Mahitaji ya wote kwa pamoja ni nguo.
![]() |
MdakiJunior - Kupata Wazo Zuri La Biashara |
Nina wazo lakini je, hizi huduma zipo katika eneo hili?
Kama wazo ulilonalo la biashara hakuna yule amelianzisha katika eneo lako basi huo ndio muda muafaka wa wewe kufanya yako. Kama limeanzishwa basi acha tafuta jingine, au fanya ubunifu kwa kutoa huduma zako kwa namna nyingine zaidi.
![]() |
MdakiJunior - Kupata Wazo Zuri La Biashara |
No comments:
Post a Comment