Logo ambayo ni rahisi na inaiwakilisha vizuri biashara au kampun yako ni muhimu sana, kwani inarahisisha hata watu kuweza kutambua biashara yako au kukufikiria wewe mara tu waonapo logo yako. Hivo katika kuhakikisha biashara yako inakuwa na inawafanya watu wavutike kwako ni muhimu kutengeneza logo ambayo inaendana na biashara au huduma ambayo unaitoa na pia logo hiyo inaiwakilisha kikamilifu biashara yako.
Pia ni muhimu kuzingatia vitu kama,
- Ni jinsi gani logo yako inaonekana kwenye bidaa
- Itaonekana vipi kwenye matangazo na material mengine
- Ni jinsi gani inaweza kuunganisha brand zako nyingine kwa urahisi.
Kwa sababu logo yako ndio kitu cha kwanza ambacho mteja wako kuona mara aonapo bidhaa yako au anaapoona bidhaa yako kwa mara ya kwanza.
Ni Zipi Aina Za Logo?
Zifuatazo ni aina za logo na huenda umewahi kukumbana nazo katika maisha yetu ya kila siku.
1. Symbol or Icon (Alama au Icon) - Logo hii huiwakilisha kampuni katika hali ya kawaida ila kikamilifu. Kampuni huweza kuwa na logo moja lakini hutengeneza aina nyinginezo za logo kuweza kufanya mabo yawe safi na kuiwakilisha kikamilifu kampuni husika.
Mfano mzuri wa logo hii ni: Apple,
![]() |
Apple Symbol Logo |
2. Word Mark (Logo ya Maneno) - Hizi ni logo ambazo zimetengenezwa kwa maneno ambayo yanakuwa yamerembwa kwa typeface tofauti tofauti au moja kuweza kuiwakilisha kampuni kikamilifu. Mfano mzuri ni logo ya Millardayo, facebook, Sony.
![]() |
MillardAyo Word Mark Logo |
3. Letter Mark (Logo ya Herufi) - Logo za namna hii huweza kutumia herufi za mwanzo za jina la kampuni, biashara au brand. Kampuni nyingi ambazo hutumia logo hii hutokana na jina la kampuni yaani herufi za mwanzo huweza kukaa vizuri na kutengeneza logo safi kwa matumizi.
Mfano mzuri ni logo ya hp computers,.
![]() |
Hp Letter Mark Logo |
4. Combination Mark (Mchanganyiko Alama na Maneno) - Hii ni aina ya logo ambayo hutumiwa kwa kiasi kikubwa na kampuni nyingi. Logo hizi hujumlisha herufi au alama na maneno mengine.
Mfano mzuri wa logo za namna hii ni Azam, Vodacom, Airtel.
![]() |
Azam Combination Mark Logo |
5. Emblem - Logo hii hufungia jina la kampuni ndani ya design au mduara. Logo hii mara nyingi huweza kutumiwa na shughuli za kiofisi hasa taasisi kama vile mashule. Mfano mzuri wa logo za namna hii ni kama vile Logo ya Udom (The University Of Dodoma).
![]() |
Udom Emblem type Logo |
Unahitaji Logo? Umepata kujua ni aina gani ya Logo Unahitaji? Karibu sana, nadesign na kutengeneza Logo Kwa matumizi yako. Tafadhali kama upependa post hii share na rafiki kwenye mitandao ya kijamii kwa kubofya link za kushare hapo chini.
Vizuri Sana Kaka umefungua wengi baadhi ya wateja wanakua wagumu kielewa lkn kama mtu akisoma makala hii nadhani atapata kitu lkn pia napenda tuandalie makala itakayo elezea jinsi ya kupanga bei ya logo ni vitu gani hasa vinaangaliwa
ReplyDeleteAsante kwa kunielewesha I was knew nothing
ReplyDelete