Full width home advertisement

Graphics

Tech News

Post Page Advertisement [Top]

Bingo..! bila shaka upo google muda huu na unatafuta namna ya kutoa password kwenye simu ambayo huenda ukawa umesahau password yake haijalishi ni kwa bahati mbaya au makusudi. Ni kweli password zinasahaulika na mara nyingi inatokea pale unapokaa kwa muda mrefu bila kutumia simu yako. Basi usiwe na wasi wasi simu yako itafunguka na utaweza kuitumia tena, haina haja kwenda kuflash.
 Itakuwa ni ajabu sana na kitu kisichokubalika kwa tafiti zilizofanywa kwa binadamu wa sasa kuweza kukaa muda mrefu bila ya kuwa na mawasiliano yaani simu. Kitu hiki huenda wanaokiweza hadi sasa ni sokwe tu ambao kwao mstuni teknolojia bado ni tete.

Mambo ya kuzingatia
Onyo! Hakikisha simu yako ina chaji ya kutosha. La sivo ichajishe hadi ijae. Process hii pia itafuta data zote kwenye simu yako hivo basi hakikisha umesave data zako za muhimu kama picha, video na contacts kwenye computer au kwenye simu nyingine. Usitoe battery wakati hatua inaendelea.  

Tukiacha bla bla,,, ni vipi naweza kutoa password
Ni swali ambalo utakua unajiuliza hadi sasa, amini usiamini password zinatoka na yakupasa kufanya yafuatayo.

Kwa watumiaji wa Tecno
1. Zima simu yako tumia kitufe cha kuzima simu na izime kabisa.
2. Baada ya kuwa umeizima iwashe na fanya yafuatayo kabla haijawaka kabisa.
Bonyeza kitufe cha kuzima au kuwasha  kisha kitufe cha kupunguzia sauti kwa pamoja. Hadi pale utapoona screen maalum imetokea.
Baada ya kuwa umeizima ikiwa inawaka bonyeza kitufe chakuzima na kupunguza sauti.
3. Utaona options tumia Volume up au Volume Down kuweza kwenda juu au chini, tumia Kitufe cha kuzimia simu kuweza kuchagua.
Tumia kitufe cha sauti kuongeza na kupunguza kushuka chini au kupanda juu na kitufe cha kuzima kufanya chaguzi.
4. Chugua sehemu imeandikwa Factory Reset au Wipe data 
5. Baada ya hapo simu process ya kufuta data zote itafanyika na password itakua imetoka. Na simu yako itakuwa kama mpya.


Kwa watumiaji wa Simu Nyingine
Kama unatumia simu nyingine fanya haya.
1. Zima simu yako tumia kitufe cha kuzima simu na izime kabisa.
2. Baada ya kuwa umeizima iwashe na fanya yafuatayo kabla haijawaka kabisa.
Bonyeza kitufe cha kuzima au kuwasha    kitufe cha home na kile cha kuongezea sauti  kwa pamoja hadi pale utapoona screen maalum imetokea.
Kama hakuna kitufe cha home kwenye simu yako basi tumia hizo mbili.

3. Agalia screeen inayojitokeza, kama hakutakuwa na screen rudia hatua namba 1 na  namba 2 hapo juu.
4.  tumia Volume up au Volume Down kuweza kwenda juu au chini, tumia Kitufe cha kuzimia simu kuweza kuchagua.
5. Chugua sehemu imeandikwa Factory Reset au Wipe data au  Delete all user data au sentesi nyingine kama hiyo.

MUHIMU!! Hadi hapo nina uhakika umefanikiwa kufanya hivo. Niandikie comment hapo chini kama utapata tatizo lolote, pia share kwa rafiki zako waweze kupata ujuzi huu.




Mawasiliano:
Instagram: mdaki.jr
Phone: +255 628 420 222

42 comments:

  1. Mbona Mimi nimejaribu kwenye TECNO S2 lakini imeshindikana na imeleta FASTBOOT ,Me sijajua shida nini?

    ReplyDelete
  2. Simu yang haisapoti kwenye computer inapelek chanji tu shida ni nin

    ReplyDelete
  3. Bigup broo asante sana imekubali ungeweka kapu la sadaka kabisa tutoe sadaka tuliosaidika

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona cm inazima na kuwaka haileti hayo mmaneno

      Delete
    2. Mbona mimi najaribu inashundikana au paka utoe laini

      Delete
    3. kaka me mwenyewe nimejaribu Imegoma spark 2 inaleta alama ya chaji alaf inaandika fast boost nikijarib kingine inakua inazima zima

      Delete
  4. Mbona ina leta fastboot tu

    ReplyDelete
  5. Daa mimi nimeweza ahsante sana

    ReplyDelete
  6. Simi yangu mm inaweka namba sita je nafanyaj

    ReplyDelete
  7. Simu yangu imegoma yani inaandika tekno alaf inazima then inawaka tena

    ReplyDelete
  8. Mm nimejaribu kwa cm njia zote lkn njia y pili imenipa muongoz n nikafunguka lkn bado haijakubali ...cm yangu ni ARROWS

    ReplyDelete
  9. Me nimeshndwa kwa vivo

    ReplyDelete
  10. Kwa Nokia za batman inakuwaje

    ReplyDelete
  11. Mbona mm umegom nifanyej

    ReplyDelete
  12. Mm imegoma ni Aina ya vivo haifunguki nimesahau Pn nimepitiwa njia zote

    ReplyDelete
  13. nataka kutumia pc kuifungua

    ReplyDelete
  14. Imemaliza lakini unataka niweke email na Mimi nimesahau nifanyeje

    ReplyDelete
  15. Mi nahitaji kuhamisha picha na password nimesahau nifanyaje

    ReplyDelete
  16. Jmani mm nimesahau paswd nimefanya kama I navyoelekeza lakini inaandika infix na kuzima Nisaidie

    ReplyDelete
  17. Kwa Nokia mbona inakataa

    ReplyDelete
  18. Kaka mim yangu imekataa ni oppo

    ReplyDelete
  19. eee bro Kwa iPhone inakubali kweli mana Nina mmashaka

    ReplyDelete
  20. Mbna mwisho inataka niingize previous password na sikumbuki

    ReplyDelete
  21. Mi nimefanya kama alivyoelekeza kwa Infinix smart8 ila sijafanikiwa nisaidie

    ReplyDelete
  22. Mkuu nimefika Hadi ktk maandishi yaliyo_andikwa" wipe data/factory reset" baada ya hapo ndo sijui nifanyaje au una_shusha Tu Hadi hapo alaf unaacha unaendelea yenyew?msaada mkuu

    ReplyDelete
  23. Mimi nmejalibu inaleta machagulio matatu ,recovery mode ,fast boot ,Normal boot apo naomba unielekeze mana nmexhindwa

    ReplyDelete
  24. Simu yangu oppo imegoma mpka leo kutoka ukitada kuitoa inafika wakata screen aitach

    ReplyDelete
  25. Mbna kweny oppo inadai passcode

    ReplyDelete
  26. Nimejaribu kwenye Huawei imekataa shida ni nini

    ReplyDelete
  27. Mbona SM yangu imekata kuleta hayo maandsh ni infinx

    ReplyDelete
  28. Cm Tecno smat Imel izo674899306634357 nimesahau passwerd

    ReplyDelete
  29. Mbona nimejaribu kwenye cm ya nokia aileti Reset kama hizo imei yake ni 351345007767324

    ReplyDelete
  30. Mimi imejaribu kaka lakini bado inadai paswed ya zamani kaka nisaidie

    ReplyDelete
  31. ...nimefanya hvyo lakn inaitaj imail.au password Tena ya zaman

    ReplyDelete
  32. MM NIMEJARIBU SIM YANGU NDO KWANZA INAWAKA NA KUZIMA NA MACHAGUO HAKUNA HATA MOJA VIP NIFANYEJE MSAADA BROO

    ReplyDelete

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib