Full width home advertisement

Graphics

Tech News

Post Page Advertisement [Top]

Ninaweza sikati tamaa

Kwanini ukate tamaa? Kwanini ujione wa tofauti? Kwani wewe si kama binadamu wengine? Unaweza inuka kutoka hapo ulipo na anza taratibu. Hakika unaweza.

Yawezekana vipo vingi vikwa viavyo kurudisha nyuma, lakini njia mojawapo ya kushinda vikwazo hivo ni kutambua ni wapi vinaanzia. Huenda wewe ukawa ni kikwazo, au familia ikawa ni kikwazo, lakini sio sababu ya kukata tamaa katika maisha.

Nakupa story fupi inayo nihusu mimi? Niliwahi kuwa mtu ambae hana uelekeo maalum katika maisha. Niliwahi kukata tamaa. yamkini ningeendelea na hali ile huenda hata leo hii sisingekuwa na na nafasi ya kuandika post kama hii.

Kama unapata shida kuusu familia, marafiki, kazi au mahusiano. jaribu kufanya hata vitu kama hivi vichache.

1. Kwanza tambua sababu ya tatizo. 
Kama ni wewe basi jaribu kujirekebisha. Unaishi na wazazi ambao wawajakuzaa, ndugu unaoishi nao wanakunyanyasa, mpenzi wako amekuacha, usikate tamaa. Tumia muda mwingi kumuomba Mungu kwani ana fungu ameandaa kwa ajili yako.

 2. Jaribu kutafuta ufumbuzi wa tatizo.
Kama tatizo ni upendo basi ongeza upendo, kwa watu wako wa karibu na hata juhudi katika kufanya kazi. Hii yaweza kukuondolea baadhi ya mawazo kukuweka huru, pia inakupa nafasi ya kuanza tena.

3. Fanya kazi au jishughulishe na vitu uvipendavyo, usipende kukaa bila kufanya chochote.
Kama unakitu unaweza kufanya basi fanya usiwe mtu wa kuwa pekeako mara zote. Au kutembea tembea ovyo. Kuliko kutembea ni bora kufikiria njia za kupata pesa.

4. Usipende kusikiliza nyimbo za huzuni. 
Mara nyingi ujumbe unaotolewa kwenye nyimbo unachangia pia katika kukuweka mpweke na kuamsha hisia za kukata tamaa, hivo chagua nyimbo zenye kuchangamsha n kukujenga kimawazo.

5. Ungana na watu kujifunza vitu vipya.
Sababu nyingine kwanini watu wanakata tamaa ni kutokana na kuishi bila kushirikiana na watu wengine. Shirikiana hii itakupa nafasi ya kupata vitu vipya na njia tofauti za kuyafikia malengo.

6. Fuatilia habari za redio au hata luninga.
Pata habari, elimika, tumia elimu yako kufanya vitu vya maendeleo katika maisha yako na jamii ikuzunguukayo.

Usikate tamaa, kikwazo cha maendeleo yako ni wewe mwenyewe, japo yawezakuwa na sababu nyingine ila nyingi una uwezo wa kuzitatua. 

Amka!!


Share kwa ndugu na jamaa ujumbe huu kuwa hakuna sababu ya kukata tamaa.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib