Full width home advertisement

Graphics

Tech News

Post Page Advertisement [Top]

Elimu juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii na jinsi ambavyo inaweza kuleta madhara katika ulinzi wako binafsi pamoja na taarifa zako, ni suala ambalo watu wengi wamekuwa hawalifahamu. Hivo inakuwa changamoto kubwa katika kujilinda na utapeli pamoja na madhara mengine yatokanayo na internet.

MdakiJunior - Matumizi ya Mitandao 

Matumizi ya Mitandao.
Katika mitandao iwe ile ya kijamii au matumizi ya kawaida ya matumizi ya mtu na mtu yanatofautiana. Na kila mmoja ana lengo lake la kuwa katika mitandao. 
  1. Matumizi mazuri. Hapa ni kutumia mitandao vizuri bila kuleta madhara au uhalifu kwa watumiaji wengine wa mitandao hiyo. Mfano: Kutumia mitandao ya kijamii kwa taarifa zako wewe bila ya kutumia za mtu mwingine.
  2. Matumizi mabaya. Hapa ni kutumia mitandao kwa lengo la kuleta madhara kwa watumiaji wengine wa mitandao. Mfano: Kutumia taarifa zisizo zako katika mitandao ya kijamii au kuibia watu kwa kutumia mitandao hiyo.
Je ni mambo gani ya kuzingatia uwapo kwenye Mitandao?
i. Kuwa makini na taarifa za binafsi unazoziweka kwenye mitandao wa jamii.

ii. Ukisaidiwa kuanzisha akaunti za mtandao wa kijamii, hakikisha unabadilisha neno la siri lilotumika mara moja; neno lako la siri ni siri yako usimshirikishe mtu mwingine,
Tunza neno lako la siri unalotumia katika huduma zako za kwenye mtandao, mfano barua pepe, miamala ya kibenki.

iii. Usijibu ujumbe wowote wa barua pepe unaokueleza kuwa umeshinda bahati nasibu bila kuhakikisha uhalali wa barua pepe husika.

iv. Usijibu jumbe unazopokea kwenye akaunti yako ya barua pepe au ujumbe mfupi wa simu unaoulizia taarifa au unaokutaka kuhakiki taarifa zako binafsi za akaunti za huduma mbalimbali kwenye mtandao wa intaneti bila kuhakiki uhalali wa uhalali wa uhalali wa uhalali wa uhalali wa uhalali wa taarifataarifataarifataarifa taarifa husika husikahusika husika

v. Usifungue kiambatisho au kubofya (link) unayotumiwa na mtu usiyemjua kabla ya kuhakikisha uhalali wa barua husika au ujumbe huo.

vi. Tumia programu za compyuta za wakati na hakikisha kompyuta au kifaa chako cha kielektroniki kinatumia programu za kujikinga na virusi hatarishi.

vii. Tumia muda kujielimisha kwa kusoma taarifa mbalimbali zinazohusiana na huduma za mtandao wa intanet unazotumia. 


Ili kujiepusha kukiuka Sheria mbali mbali za mawasiliano ya mtandao, unashauriwa kuzingatia yafuatayo.
i. Usitunge na kusambaza ujumbe wa maudhi, uzushi au uchochezi,

ii. Usiendelee kusambaza ujumbe wa chuki, maudhi au uchochezi unaopokea kutoka kwa mtu mwingine. Badala yake ufute mara uupokeapo au toa taarifa,

iii. Usitembelee tovuti au blogu za ponografia/ngono,

iv. Usitengeneze akunti za mitandao ama kwa lengo la kufanya utapeli, ulaghai au kwa kutumia taarifa zisizo zako,

v. Tunza kwa usalama vifaa vya kielektroniki unavyotumia kuhifadhi kumbukumbu zako na usitumie vifaa hivi kwenye kompyuta za umma.

Faida za huduma za mitandao.
i. Hurahisisha mawasiliano.
ii. Hupunguza gharama.
iii. Huongeza ufanisi.
iv. Huokoa muda.

TAARIFA ZAIDI NA MAWASILIANO
 Pata taarifa zaidi kutoka kwenye tovuti ya TZ-CERT kwa anuani ifwatayo: www.tzcert.go.tz.
Tovuti hii pia inatoa nafasi ya kutuma na kutoa taarifa za matukio mbali mbali kwa wataalamu wa TZ-CERT unapo hitaji msaada .
 Kwa kutoa taarifa za tukio ili kupata msaada tumia anwani ya barua pepe ifwatayo: incidents@tzcert.go.tz au info@tzcert.go.tz
 Pia unaweza kuwasiliana kupata taarifa muhumi na kutoa maoni au kuuliza maswali kwa kutumia akaunti za mitandao ya kijamii zifwatazo:

Kwa mawasiliano ya simu piga: 022 2412 039 au 022 2199760-9

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib