Full width home advertisement

Graphics

Tech News

Post Page Advertisement [Top]

Modem ni kufupisho cha (Modulator Demodulator) modem ni kifaa cha network ambacho kinakusaidia kusafirisha data kwenye computer yako mfano: kwa wireless connection (WiFi), telephone nk. Zipo aina nyingi za modemu na zinatumia njia tofauti tofauti katika kusafirisha data kwenye computer yako na kukuruhusu kuwa kwenye mtandao (internet). Mfano wa modem ni kama ZTE, Huawei n,k
image
MdakiJunior - Kuunganisha internet kwa modem
Ikiwa kompyuta yako haina tatizo na modem inafanya kazi vizuri basi ukisha iweka kwenye computer yako itafanya Autoplay na itainstall madile yote ya muhimu. Baada ya hapo utaunganisha kwenye internet na inakuwa sawa.

Modem haitaki kuunganisha na internet
Ikiwa unapata tatizo la kuunganisha modem yako na internet basi jaribu kufanya yafuatayo.

  1. Kama unatumia ZTE, Huawei au modem nyingine za namna hiyo, hakikisha kwanza hardware za computer yako ziko vizuri.
  2. Angalia port uliyoweka modem kama inapitisha umeme wa kutosha, hakikisha kwa kuweka flash ikisoma bas hakuna tatizo ikikataa basi badili port.
  3. Hakikisha mahala ulipo mtandao unasoma vizuri.
  4. Angalia configuration settings hii utaipata kwenye network settings, kama kuna tatizo kwenye configuration inaweza kuwa vigumu pia kuweza kuunganisha na internet kwenye modem yako.
  5. Muda mwingine bando pia laweza kuwa ni tatizo kuunganisha kwenye internet kwa baadhi ya mitandao hivo kuwa na bando ili mambo yawe rahisi zaidi.
Kila kitu kipo sawa ila bado haitaki kuunganisha.
Muda mwingine unaweza letewa ujumbe kama huu "Your connection has been terminated by a remote computer before it has been established"
image
MdakiJunior - Modem
Jinsi ya kufanya
image
MdakiJunior - kutengeneza profile nyingine.
  1. Jarinu kubadilisha profile, na weka profile nyingine
  2. Ikishindikana tengeneza profile nyingine kwenye network settings
  3. Fungua settings nenda kwenye network settings bofya add hapo utaweka configuration nyingine.
  4. Utaweka jina la profile, pia utaweka dial number ambayo ni *99# kisha utaisevu kwingine acha kama ilivokuwa.
  5. Rudi kwenye connetion chagua ile profile uliyotengeneza na jaribu tene kuunganisha.

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib