Kama unamiliki computer ni bora pia kufahamu kuwa ni matatizo gani yanaweza kudhuru au kupunguza ufanisi wa computer yako. Computer inapopata tatizo lolote kitu cha kwanza cha kuhofia ni kupoteza data. Hakuna mtu anaependa kupoteza data ambazo amechukuwa muda mwingi katika kuziandaa au kuzitengeneza.
Hivo yajue matatizo ambayo yanaweza kupelekea wewe kupoteza data zako na ufahamu jinsi gani unaweza kujilinda na matatizo hayo.
Je matatizo gani hukumba zaidi computer?
Computer hukumbwa zaidi na matatizo yafuatayo.
1. Matatizo kwenye Hardware - hardware ndiyo computer yenyewe na inahusisha vitu vyote ambavyo unaweza kuvishika kwenye computer yako, Mfano: Hard Disk, Monitor, keyboard, mouse n.k. Hivyo patokeapo tatizo katika hardware hasa kwenye disk inaweza sababisha kutofanya kazi kwa computer yako au kupoteza data.
2. Computer kupata joto kupita kiasi (Over heat) - sababu mojawapo ya matatizo ya computer ni kuijaza application nyingi, hivo inachemka kupita kiasi na kupelekea matatizo katika computer yako. Hii pia inaweza sababishwa na kutofanya kazi kwa feni za kupozea computer yako.
![]() |
MdakiJunior - Computer Kupata Joto zaidi kupita kiasi. |
3. Matatizo ya umeme -kama hauna vitu vya kulinda computer yako ikiwa kutatokea tatizo la umeme una ailimia kubwa ya kupoteza data zako kwani kukatika kwa umeme kwa ghafla ikiwa bado unafanya kazi zako ni tatizo kubwa.
![]() |
MdakiJunior - Tatizo la umeme kukatika ikiwa unafanya kazi na computer yako. |
4. Virusi na program hatarishi kwenye computer yako - Virus ni program zilizotengenezwa ili kuweza kubadilisha utaratibu ambao unafanywa na computer na kuweka utaratibu wake mpya ambao hautambuliki na haukubaliki na computer yako. Mfano: kutengeneza files bila mpangilio, kuhamisha files, kufuta n.k
![]() |
MdakiJunior - Computer kuvamiwa na virus |
5. Kuvamiwa na wadukuzi (Hackers) - Computer yoyte iliyo kwenye Internet iko kwenye hatari kubwa ya kuvamiwa na wadukuzi. Wadukuzi wanapovamia computer yako kuna hatari kubwa sana ya wewe kupoteza data zako. Mfano: Ransomware hiiki ni kirusi ambacho kinafunga mafile ya computer yako na kukutaka utoe pesa ili kurudishwa tene kwa mafile hayo.
![]() |
MdakiJunior - Computer kuvamiwa na wadukuzi (Hackers) |
6. Matatizo katika Operating System (OS) - OS ni software ambayo ndiyo inaongoza na kuratibu mipangilio na kazi zote ndani ya computer yako. Pia inaruhusu wewe uweze kuweka application (Software) nyingine. Mifano wa operating system ni kama: Windows, Linux, Android(kwenye simu) Ubuntu. Kwa binadamu OS naweza kusema ni kama moyo. Hivo tatitizo lolote kwenye operating system yako inaweza sababisha kutofanya kazi kabisa kwa computer pengine hata kukulazimu ubadili OS na kuweka nyingine.
![]() |
MdakiJunior - Matatizo katika Operating System |
7. Uchafu unaosababishwa na vumbi au moshi - moshi au vumbi vikiingia kwenye computer yako vinaweza haribu hardware za muhimu kama hard disk. Hivo umakini unahitajika katika kutunza vifaa vyako vya computer.
![]() |
MdakiJunior - Uchafu kwenye computer |
8. Kuharibu kwa bahati mbaya kwa kutokujua ufanyalo ndani ya computer yako. Hii inatokea pale unapofanya setting ndani ya computer yako bila kujua hizo setting zinaweza leta madhara gani.
Je, nawezaje kuzuia matatizo kwenye computer yangu?
Kuweza kujizuia na matatizo kama haya fanya yafuatayo.
- Kuwa na backup ya data zako. Yaani hifadhi data zako sehemu nyingine tofauti na kwenye computer yako, ili hata tatizo likitokea mdano kuibiwa computer au kuharibika uwe na sehemu ya kupata data zako.
- Usifanya setting ambazo huna uhakika na hujui kazi zake ndani ya computer yako.
- Usipende kuiacha computer yako ikiwa inawaka kama huitumii kwa muda huo.
- Tumia program za kulinda computer yako na virus tena za wakati huo (Updated).
- Zima computer yako kwa kufuata taratibu na sio tu kubonyeza kitufe cha kuzimia.
- Linda taarifa zako za mitandaoni ikiwa ni pamoja na kutumia password ambazo sio rahisi kuzihisi ili kujilinda na wadukuzi.
- Usijibu ujumbe wa Email kutoka kwa mtu usiyemfahamu kwani anaweza kukutumia link ambayo inaweza install program ambazo zinaweza chukua taarifa zako.
- Usitumie computer yako hadi ikaishiwa chaji kabisa na kuzima yenyewe (izime ikikaribia kuisha chaji na hakikisha umefunga program zote).
- Tumia muda wako kujielimisha zaidi.
No comments:
Post a Comment