Full width home advertisement

Graphics

Tech News

Post Page Advertisement [Top]

Kumekuwa na matatizo ya udukuzi (hacking) account za instagram kila kukicha. Je, nawezaje kujilinda na janga hili? Ni moja ya swali ambalo ungependa kujiuliza kama Account yako ya instagram bado haijadukuliwa na wadukuzi. Dukua/hack ni kitendo cha kuchukua taarifa za mtu mwingine ili kuweza kupata nafasi ya kutumia huduma za mtu huyo ambaye umechukua taarifa zakeMdukuzi/hacker ndiyo huyo mtu ambaye anafanya kitendo cha kudukua  Zipo sababu nyingi zinazopelekea watu kuweza kuhack account za instagram.

Kwanini account zinadukuliwa?

  1. Kwa lengo la kujipatia pesa.
  2. Kupata Followers amabo unao kwenye account yako.
  3. Kwa lengo la kukuchafulia jina, hsa kwa wasanii wakubwa na makampuni.
  4. Kwa ajili ya kujaribu uwezo wao hao wadukuzi (hackers) kuwa wanaweza kuhack.
  5. Kwa lengo la utani hii inatokea kwa marafiki wa karibu.

image
MdakiJunior - Linda account yako isihackiwe

Nawezaje kujua kama account yangu inataka kudukuliwa?
Kama utaona miongoni mwa hivi vifuatavyo basi kuwa makini kuna hatari ya account yako kudukuliwa.

1. Pata tick ya uthibitisho wa account yako (Get a Verified Batch) hakuna ambaye hapendi kupata ile tick ya blue kwenye account yake, ila kwa bahati mbaya hiyo tick huwa haitolewi hovyo hovyo. Hivo kuwa makini na link inayokwambia pata verified batch.
Tazama mfano hapo chini.
image
MdakiJunior - Link fake ya jinsi ya kupata batch (Tick ya blue)

image
MdakiJunior - Link fake ya jinsi ya kupata batch (Tick ya blue)

2. Tumiwa Email ya tahadhari (Exortic Performance) kuwa juu ya content unazoziweka instagram. Hapa utatumiwa email kwenye account yako na watakutaka uingie kwenye account yako kwa kuweza taarifa zako za muhimu. Wanajua kabisa kuwa huwezi kufungua kitufe cha (View Details) hasa kwa account za Google, kwani huwa taarifa za mtu alietuma email zimefichwa hadi ufungue. Hivo ukijibu email hiyo bila kuangalia mtu aliyetuma unaweza kuhatarisha account yako.
Angalia mfano hapo chini.
image
MdakiJunior - Email ya tahadhari

3. Phishing hapa mdukuzi anakutumia page inayofanana na ile ya instagram kwenye email yako au kwa njia ya ujumbe ukiwa instagram. Na ukijaribu kuingia kwenye account yako kutumia ukurasa huo anaweza letewa ujumbe wa tahadhari (error messege) na hapo taarifa zako zinakuwa zimechukuliwa tayari.

Je nawezaje kuirudisha account yangu iliyo dukuliwa?
Kwa instagram fungua instagram help center baada ya hapo fuata utaratibu ambao utapewa na kama account yako imedukuliwa pia unaweza toa taarifa pale.


Tazielezea Tools ambazo hackers wanatumia ili kuweza kuhack Account mbali mbali.
Endelea kutembelea Blog yangu.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib