Full width home advertisement

Graphics

Tech News

Post Page Advertisement [Top]

Windows 10 ni Operating System ambayo imetengenezwa na Microsoft kama mbadala wa Windows 7 na Windows 8. Kiukweli utumiapo windows 10 japo iko vizuri kwa upande wa Ulinzi n.k vipo vitu vya kufanyia marekebisho mfano hili swala la lazima la kufanya Auto update. Japo ni muhimu kuwa na updates kwa jili ya Security lakini muda mwingine updates zinafanya mabadiliko na muda mwingine kuleta hitiliafu mbali mbali, Mfano: kwenye driver.

Muda mwingine unaweza kuwa umeunganisha computer yako kwa Wi-Fi ya simu yako, ikiwa umepewa Bandwidth ya 300Mb na mtandao wako ila updates zinahitaji 4Gb hivo unajikuta ndani ya dakika 3 hauna tena bando, kiukweli inachosha. Takua nikitupa trick kuhusu windows 10 na jinsi gani ya kuitumia bila wasi wasi.


Natumia Windows 10 Nawezaje kutoa Auto Updates.
Unaweza kutoa Auto Updates kwa kutumia Group Police Edit au kwa kutumia Metered Connection ni rahisi fuata hatua na angalia picha ili kwenda sawa.
1. Fungua CMD (Command Prompt) kwenye Computer yako.
Bonyeza Windows Key na R kufungua Run kama hivo
2. Tumia Windows Key kwenye keyboad yako na button R kisha andika CMD.
3. Ukishafungua CMD andika gpedit.msc command.
4. Fungua Computer Configuration kisha Administrative Templates Utaenda kwenye All Settings kama inavyo onesha kwenye picha hapo chini.
Group Policy Edit Window 
5. Kwenye List ya All Settings tafuta Configure Automatic Update. Double click kuifungua. Mkono wa kushoto juu utaona sehemu imeandikwa Enable, kama bado ipo enables. Unaweza kushuka chini kidogo na kufanya settings za vipi unataka Updates ziweze kupatikana kwenye column ya kwanza kushoto baada ya hapo utabofya Apply na Ok kufanya mabadiliko.
Configure Automatic Updates
6. Au unaweza kuweka Disable kama hutaki notification za ku update mara kwa mara. kisha Apply na Unaweza restart computer yako.


Hapo utakua umefix tatizo la auto updates kama unatatizo kuhusu Windows 10 niandikie kwenye comment hapo tajitahidi kutafuta ufumbuzi. Usikose Post inayofuata kuhusu windows 10.

MUHIMU: Please Share na marafiki post hii.




Mawasiliano:
Instagram: mdaki.jr
Phone: +255 628 420 222

3 comments:

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib