Full width home advertisement

Graphics

Tech News

Post Page Advertisement [Top]

Email ni kifupisho cha "ELectronic Mail" ni moja ya vitu vya muhimu sana kwenye internet. Katika ulimwengu huu wa sasa ambapo Sayansi na Teknolojia vimechukua nafasi kubwa, ni muhimu sana kuwa na Email account. Email ina faida nyingi sana na chache nimezielezea hapo chini.

Faida za Email Account.
1. Inakusaidia kutuma na kupokea ujumbe kutoka kwa mtu yeyote mwenye Email account na ambaye ana Email yako.

2. Email inasaidia katika kununua bidhaa mtandaoni na kupata huduma nyingine za kielectronic. Mfano: Ebay Amazone n.k.

3. Email pia inatumika kama utambulisho wako uwapo kwenye internet.

4. Emil pia inatumika katika usajili wako kwenye mitandao ya kijamii n.k.
MdakiJunior - Kutengeneza Email


Mambo ya muhimu
1. Uwe na Computer ili iwe rahisi.

2 Uwe na namba ya simu.
3. Password imara.

Jinsi ya Kutengeneza Email
Kutengeneza email ya google utafungua Browser yako, Mfano: Google Chrome, Operamini, UC Browser au nyingine yoyote.
1. Ukishafungua utaandika www.gmail.com
Kama ndo kwanza unaanza kufungua Account utabonyeza sehemu imeandikw More Options 
MdakiJunior - Tengeneza Email - Bonyeza More Options

MdakiJunior - Tengeneza Email - Bonyeza Create Account

2. Weka taarifa zako za muhimu baada ya kubonyeza Create Account. Kama vile Jina kamili, username ambayo ndio itakuwa Email yako pia unaweza ibadilisha. Password, Tarehe ya kuzaliwa, Jinsia yako, Namba yako ya simu(Ambayo pia unaweza ijaza kwa baadae unaweza acha usijaze kitu) na Email ambayo unatumia kwa sasa (Sio lazima ujaze nafasi hii waweza iacha wazi.)
MdakiJunior - Tengeneza Email - Bonyeza Weka Taarifa Za Muhimu

MdakiJunior - Tengeneza Email - Bonyeza Kubaliana na vigezo na masharti.

3. Hapo unakuwa umemaliza kutengeneza Email yako. unaweza kuanza kufurahia huduma za Google kama Kutengeneza blog, kutengeneza YouTube Channel na mengine mengi.
MdakiJunior - Tengeneza Email - Unakuwa umemaliza






6 comments:

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib