Full width home advertisement

Graphics

Tech News

Post Page Advertisement [Top]

Je unajua watanzania wanaandika nini wanapokua kwenye kutafuta mada au kitu chochote kwenye google, yahoo, au search engine nyingine unazozifahamu? Nimejaribu kulifanyia uchunguzi hili na nimeona kwa asilimia kubwa. Watanzania wanatafuta mada ambazo kimsingi hata kuzielezea inakua shida kidogo.

Binafsi sikuweza kuamini, kwani nilitegemea kuona watu wanatafuta vitu vya msingi kama vile "Jinsi ya kufanikiwa kibiashara", "Jinsi ya kupata wazo zuri la biashara", "Nawezaje kuwa mtu mwenye mafanikio" na mada nyingine kama hizo.

Ila katika pita pita zangu nikatembelea ukurasa ambao unaonesha watu wanapokua kwenye engine kama google wanatafuta nini. Hapo ndipo nikakutana na hili janga, watanzania tuna safari ndefu zaidi katika kufikia maendeleo kama vitu vyenyewe tunavojifunza kutoka kwa wenzetu ni matusi tu na sio vitu vya kujenga.

Mambo ambayo yasiyo ya msingi yanapewa kipaumbele sana kuliko mambo ambayo huenda kama tutayazingatia tunaweza fanikiwa zaidi. Vijana wanatumia muda mwingi zaidi katika kutafuta mada ambazo hazina maaana kwakweli inasikitisha zaidi. 



Mdaki Junior - Mada ambazo zinatafutwa sana kwenye internet



Mabadiliko yanahitajika zaidi na kujifunza vitu vipya kila siku na sio tu vitu vipya bali vitu vipya vyenye kujenga. Na sio tu tunalalamika kuwa kazi hakuna ajira ni kwa wazee tu, hapana vijana inabidi tubadilike na kuanza kufanya vitu ambavyo vitapelekea kuwa na maamuzi mazuri katika maisha.

Mdaki Junior - Nchi zinazohusika.


No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib