Nawezaje kupata mafanikio? Maisha ni kama safari. Na katika safari yapo mengi ya kupambana nayo. Mungu ameshapanga kila kitu katika maisha yako, hivo haina budi kujipa moyo na kuamini kuwa kila jema utendalo limepangwa na Manani.
Unaweza ukiamini, utamaliza ukiwa ni mtu wa kutamani kuyafikia Malengo. Utafanikiwa ukifanya kazi kwa nidhamu na bidii. Kwa mtazamo wangu hua naamini kila nafasi ni fursa ya kufanya maamuzi ya kujenga maisha kuwa bora zaidi.
Wewe hauko kama mimi, lakini hatuna tofauti sana kuusu imani zetu, kila mtu anacho kile anachokiamini kuwa ni sahihi, hapa namanisha imani ya kimtazamo wa kutatua na kupambana na hali zetu za kila siku.
Ili kuweza kufanikiwa katika safari yako yafuatayo ni muhimu katika njia hiyo.
1. Mtangulize Mungu katika kila jambo lako.
2. Jifunze kutoka kwa watu waliofanikiwa.
3. Tengeneza plan za kila mipango yako unayotaka kufanya.
4. Fanya kazi katika mipango yako, usiyumbe.
5. Weka malengo, na fanya mikakati madhubuti ya kufikia malengo yako.
6. Jenga timu ya faida.
7. Fanya kazi kama timu, ikiwa unamalengo makubwa zaidi.
8. Sikika, tafuta njia za kuweza kusikika kama mipango yako inahitaji kufanya hivo.
9. Kuwa mkweli na fanya kila jambo kwa kuzingatia malengo yako nasiyo ya mtu mwingine.
10. Fanya kazi kwa bidii.
Mwisho japo sio hitimisho, pata muda wa kupumzika na kufurahi na watu wako wa karibu.
![]() |
Mafanikio Yangu Safari Yangu |
No comments:
Post a Comment