Blog ya muziki ni ya aina yake ambayo inakupa nafasi ya kuweka muziki kwa ajili ya watu kudownload. Unaweza kuweka Audio na hata video za Youtube. Cha msingi uwe na Email ya Google yaani Gmail Account kama hauna Email ya Google usijali. Nimeelekeza namna ya kutengeneza. Sio lazima uwe na uwezo wa HTML language ila ni vizuri ukiwa na ujuzi wa awali.
Je Natengeneza vipi Blog?
Ni rahisi sana kwani ukiwa na Email ya google unaweza Tengeneza Blog nyingi upendavyo.
Fuata hatua hizi rahisi kuweza kutengeneza blog.
1. Kwanza Tengeneza Blog.
2. Fungua www.blogger.com kwenye address bar ya Browser yako au sehemu ya kusearch.
3. Baada ya hapo utafuata taratibu hizi.
![]() |
MdakiJunior - Tengeneza Blog |
Taratibu za kufuata
Baada ya kufungua blogger.com, utabonyeza kitufe kilichoandikwa Create Your Blog
![]() |
MdakiJunior - Tengeneza Blog - Bonyeza Kitufe Cha Create Your Blog |
Kisha utaweka jina ambalo ungependa lionekane kwa watu wako ambao wanatembelea Blog yako. Kisha utaendelea.
![]() |
MdakiJunior - Tengeneza Blog - Weka Jina. |
Nenda hadi kwenye Kuanzisha Blog Yako (Create Your Blog)
![]() |
MdakiJunior - Tengeneza Blog - Bonyeza Create Your Blog (Anzisha Blog Yako) |
Baada ya hapo utapelekwa kwenye window ambayo utatakiwa kuweka Kichwa (Heading ya Blog Yako). Anwani au Address ni URL ya Website yako (Ni vizuri ukaweka anwani ambayo inafanana na Kichwa cha Blog yako).
![]() |
MdakiJunior - Tengeneza Blog - Weka Kichwa au Jina la Blog yako na Address |
![]() |
MdakiJunior - Tengeneza Blog - Hapo Blog Imekamilika. |
Jinsi ya kuweka Post Unaweza bofya Kitufe cha Chapisho Jipya au New Post
![]() |
MdakiJunior - Tengeneza Blog - Kutengeneza Post. |
MUHIMU:
Sor me nataitaj kujua jinc ya kutengeneza app
ReplyDeleteSor me nataitaj kujua jinc ya kutengeneza app
ReplyDeleteNi jambo zuri ila kama unahitaji jua namna vile unaweza tengeneza app, inabidi kwanza ujue unahitaji kutengeneza app ya platform gani yaani Android, ios, au ipi.
DeletePia uwe na uelewa wa programming language ambayo utatumia. Mfano: java, android, c++ na nyingine.
Turudi kwenye kutengeneza App, je unauelewa wa hizo language nilokutajia hapo juu?
safi sana ila sijajua jinsi ya kuingiza nyimbo kwenye blog bado
ReplyDeleteMimi blog ninayo lakini naitaji ku post wimbo mtu aki sachi uwonekane lakini aikubali kupakia
ReplyDeleteI like it
ReplyDeleteNami ninayo lakini haina muonekano mzuri hata! 😥
ReplyDelete